Tundu Lissu atakiwa kuripoti kituo cha polisi Kilimanjaro

0
42

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ametakiwa kuripoti kituo cha polisi mkoani Kilimanjaro kwa ajil ya mahojiano juu ya tuhuma za kukaripia/kugombea askari polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ametoa agizo hilo leo na kusema kuwa hakuna mtu yeyote aliyepo juu ya sheria.

“Tumeona mara kadhaa Tundu Lissu anagomba na viongozi wa polisi… Jeshi la polisi limepewa wajibu wakulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na jeshi la polisi.”

Sirro amesema kuwa mwanasiasa huyo anatakiwa kuripoti kitu cha polisi ili aeleze aliyoyafanya jana (Septemba 30, 2020).

Aidha, Sirro amewataka wanasiasa wote kuhakikisha wanazingatia amani, utulivu na kuheshimu sheria kwani bila ya hivyo hawatoweza kufanya siasa.

“Inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo kuna viongozi wachache wanataka fujo ifanyike ili uchaguzi usifanyike, hiyo nafasi hawana,” amesisitiza Sirro.

https://twitter.com/swahilitimes/status/1311707121273245700?s=20

Tundu Lissu yupo mkoani Kilimanjaro akiendelea na kampeni za kuomba ridhaa kwa wananchi wamchague aiongoze Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

Send this to a friend