Tunisia yawafunga jela wanawake tisa kwa ugaidi

0
40

Tunisia imewafunga jela wanawake tisa wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge la kigaidi ambao wanatuhumiwa kupanga njama ya kumuua waziri wa serikali ya nchi hiyo.

Hukumu hizo zilitolewa na mahakama katika mji mkuu wa Tunis ikiwahukumu miaka 25 wanawake wawili wanaodaiwa kuwa viongozi wa kundi hilo huku wengine saba wakihukumiwa kifungo cha miaka mitatu na miaka 14.

Imeripotiwa kuwa wanawake hao walishtakiwa mwaka 2016 baada ya ripoti zilizooneka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu jaribio la kumuua waziri wa mambo ya ndani wa zamani, Hedi Majdoub wakati ya ziara ya wazazi wake, japokuwa ofisi yake ilikanusha.

Mvulana wa miaka 17 ashikiliwa kwa kuwapa mimba wanawake 10

Kituo kimoja cha redio kiliripoti kwamba mmoja wanachama wa genge hilo alikuwa akiishi karibu na wazazi wa Majdoub, na kudaiwa kutoa taarifa zinazohusu ziara zake.

Send this to a friend