Tuzo za TFF kutolewa Julai 7

0
87

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kutoa tuzo za msimu wa mashindano ya shirikisho zitakazofanyika Julai 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimegawanyika katika makundi mbalimbali zikiwemo tuzo za kikanuni za mashindano, tuzo binafsi za wachezaji na waamuzi, tuzo za heshima na tuzo za kiutawala, zikihusisha wasimamizi wa mpira wa miguu na wadau wengine waliotoa mchango wao katika mchezo huo.

Aidha, shirikisho limesema mbali na tuzo za kawaida zinazohusiana na mashindano, pia kutakuwa na tuzo binafsi 57, zikiwemo zile zinazotolewa kwa mtu zaidi ya mmoja kama vile seti bora ya waamuzi, kikosi bora cha ligi kuu ya wanawake na Kikosi bora cha Ligi Kuu ya NBC.

TFF imeongeza kuwa kwa mara ya kwanza katika sherehe za msimu huu kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya ‘Championship’ na mchezaji bora wa ‘First League’.

Send this to a friend