Twitter kuongeza idadi ya herufi kufikia 2,500

0
37

Mtandao wa kijamii wa Twitter umepanga kuongeza idadi ya herufi kutoka 280 iliyopo sasa hadi kufikia 2,500 ili kuwapa nafasi watumiaji kuchapisha picha na maneno mengi zaidi kwa wasomaji wao.

Kipengele hicho kitachukua muda wa miezi miwili pamoja na kuhusisha kikundi kidogo cha waandishi kutoka nchini Canada, Ghana, Uingereza na Marekani.

Aidha, hatua hiyo inaelezwa kuwa ni muhimu kwa Twitter kwani itawahimiza watumiaji kusalia kwenye mtandao huo badala ya kuunganishwa na tovuti zinazotoa maelezo marefu.

Hata hivyo, Profesa wa Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Illinois Urbana-Champaign, Dk Nikki Usher wakati akizungumza na chombo cha habari cha BBC amedai moja ya mambo anayoyajua ni kwamba watu hawapendi kusoma maandishi marefu mtandaoni.

Send this to a friend