Twitter yazindua huduma ya kutuma ujumbe kwa sauti

0
39

Kwa miaka ya hivi karibuni mtandao wa Twitter umekuwa ukiongeza nguvu kuhakikisha kuwa inadhibiti kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi, na sasa imekuja na huduma mpya ya kutuma jumbe kwa njia ya sauti.

Juni 17 mwaka huu kampuni hiyo iliwaruhusu baadhi ya watumiaji mfumo endeshi wa iOS (kutoka Apple) kuunda jumbe (create tweets) kwa kutumia sauti zao, ambapo kwa siku za usoni watumiaji wote wa iOS wataweza kutumia huduma hiyo.

Hata hivyo baadhi ya watumiaji wamesema kuwa maboresho hayo huenda yakawa na madhara zaidi kwa kusambaza jumbe zenye chuki ambazo zitakuwa ngumu kutambua kwa haraka kama ilivyo jumbe za maneno.

Msemaji wa Twitter amesema kuwa wataweka mfumo wa uangalizi kabla ya kufanya huduma hiyo kuwa kwa watu wote.

Ameongeza pia watumiaji wa mtandao huo hawataweza kutumia sauti kujibu jumbe za watu wengine.

https://twitter.com/Twitter/status/1273306563994845185?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1273306563994845185&ref_url=https%3A%2F%2Fcitizentv.co.ke%2Fnews%2Ftwitter-will-now-let-you-tweet-with-your-voice-336042%2F

Kuweza kutuma ujumbe kwa njia ya sauti unatakiwa kubonyeza alama yenye mawimbi kwenye uwanja wa kuandika ujumbe na kuanza kuzungumza. Ujumbe mmoja utakuwa na sekunde 140, ambazo ni sawa idadi ya herufi/alama zilizokuwa zikitumiwa na mtandao huo kipindi cha nyuma. Hata hivyo, ukizungumza zaidi ya sekunde 140, mtandao utatengeneza uzi (thread) wenyewe.

Twitter imesema kuwa inaamini maboresho hayo yataongeza ladha ya ubinadamu, na kuwezesha kutuma ujumbe mrefu zaidi kwani alama 280 wakati mwingine hazitoshi.

Send this to a friend