Uber yashtakiwa na wanawake 550 kwa unyanyasaji wa kingono

0
19

Kampuni Uber inashtakiwa na wanawake 550 wanaodai kufanyiwa vitendo viovu na madereva walipokuwa wakitumia huduma ya usafiri.

Malalamiko hayo yaliyowasilishwa Jumatano katika mahakama ya Marekani, yanajumuisha malalamiko mbalimbali yakiwemo utekaji nyara, unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kingono, ubakaji, pamoja na kunyanyaswa na madereva hao.

Kulingana na malalamiko hayo, mashambulio hayo yanayodaiwa yalifanyika katika majimbo kadhaa nchini Marekani, mpaka sasa kesi nyingine 150 zinafanyiwa uchunguzi.

Msemaji wa kampuni hiyo amesema unyanyaji wa kijinsia ni uhalifu wa kutisha na kama kampuni inachukulia kwa uzito kila taarifa wanayoipokea.

“Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko usalama, ndiyo maana Uber imeunda vipengele vipya vya usalama, imeanzisha sera zinazowalenga waathirika, na kuwa wazi zaidi kuhusu matukio mabaya. Ingawa hatuwezi kutoa maoni kuhusu kesi hizo, tutaendelea kuweka usalama,” amesema.

Kulingana na ripoti ya usalama iliyotolewa mwaka 2014, kampuni hiyo ilipokea ripoti 3,824 za unyanyasaji wa kijinsia, ambazo ni pamoja na ubakaji na udhalilishaji wa kingono ambapo ilikiri kufahamu kesi hizo lakini hawakuchukua hatua.

Send this to a friend