UBIA WA TWIGA WAONESHA ATHARI CHANYA ZA KIMAGEUZI ZA UCHIMBAJI MADINI, YASEMA BARRICK

0
38

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Tanzania, Septemba 29, 2023 – Kampuni ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD) (TSX:ABX) na serikali ya Tanzania zimedhihirisha jinsi uchimbaji madini unavyoweza kuwa na manufaa makubwa pale wachimbaji madini na serikali wenyeji wanaposhirikiana katika kuleta thamani endelevu kwa wadau wote, anasema Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Mark Bristow.

Akizungumza na vyombo vya habari hapa leo, Bristow alisema ubia mwanzilishi wa Barrick na Serikali uliyoiunda Kampuni ya Twiga ambamo pande zote mbili zinagawana kwa usawa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya North Mara na Bulyanhulu, unapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa ni ubia wenye mafanikio makubwa, hasa katika nchi zinazoendelea. Aidha, si tu kwamba Barrick sasa ndiyo mchangiaji mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania kupitia kodi, mishahara, gawio, malipo kwa wasambazaji wa ndani, na uwekezaji katika miradi ya jamii, bali pia kampuni hiyo imethibitisha kwa makampuni mengine ya kimataifa ya madini kuwa nchini humu kunawekezeka.

Tangu mwaka 2019 ilipoichukua migodi hiyo miwili iliyokuwa imekufa, Barrick imeibadilisha na kuifanya kuwa ya kiwango cha kimataifa na hivyo, kutoa mchango mkubwa katika faida halisi ya kampuni. Aidha, katika kipindi hicho, kampuni hiyo imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika uchumi wa Tanzania, huku mwaka huu Twiga ikitambuliwa kuwa mlipaji mkubwa wa gawio kuliko makampuni yote ambayo serikali ina maslahi nayo. Migodi ya Barrick hutumia asilimia 84 ya bajeti yake ya manunuzi kwa makampuni ya ndani huku asilimia 96 ya nguvukazi yao ikiwa ni wananchi wa Tanzania.

Kwa moyo huo huo wa ushirikiano, Barrick imetoa dola milioni 40 kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na dola milioni 30 zaidi katika uboreshaji wa suhula za elimu ya juu nchini.

Migodi yote miwili iko katika mwelekeo mzuri wa kuufikia mwongozo wake wa uzalishaji wa mwaka 2023 na utafutaji wa madini pia. Kwa sasa, utafutaji madini katika maeneo yote ya Barrick yaliyopewa leseni umeonesha fursa mpya za maendeleo katika maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mgodi mpya wa chini ya ardhi huko North Mara.

“Ubia wetu wa Twiga si tu kwamba unaongeza thamani katika uchumi wa Tanzania bali pia katika ubora wa maisha ya jamii zinazoizunguka migodi yetu na ambayo iaendelea kustawi. Kuendelea kwetu kujihusisha na jamii hizi na viongozi wao wa vijiji, AZISE za maeneo hayo pamoja na mashirika ya haki za binadamu kunaonesha falsafa ya Barrick ya ubia na dhamira yetu ya dhati ya kuzingatia haki za binadamu katika maeneo tunayofanyia kazi,” alisema Bristow.

Send this to a friend