Uboreshaji mkubwa katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini kuwapa wateja tija zaidi uko njiani

0
25

Tanzania inashuhudia ukuaji mkubwa wa maendeleo ya kiteknolojia ambao unaonekana wazi katika ongezeko la idadi ya watu waliounganishwa na mawasiliano kutumia huduma za intaneti. Kiini cha mabadiliko hayo ni teknolojia ya simu za mkononi, ambayo imewezesha kuwaunganisha watu na kutoa huduma za intaneti kuliko ilivyowahi kuwa hapo awali.

Ni ukweli pia usiopingika kuwa kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi ndizo muhimili mkuu wa mabadiliko na teknolojia hii. Uwekezaji mkubwa unaoendelea katika miundombinu ya mitandao ya simu na huduma ni ushahidi wa ushiriki wao katika kufikia malengo ya maendeleo ya nchi.

Kwa mfano, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kampuni moja tu Tigo Tanzania imewekeza takribani shilingi za kitanzania trilioni moja katika kuhakikisha kuwa miundombinu yake inakuwa ya kidijitali na bora zaidi ikiwa ni njia ya kuboresha huduma zake lakini pia kuhakikisha inachangia harakati za nchi kufikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Tigo Tanzania imejipambanua kuwa inafanya kazi katika kujenga maisha ya kidijitali nchini Tanzania na utendaji kazi wao hadi leo unaonesha nia yao ya dhati kufanikisha hilo. Ikumbukwe kuwa Tigo ni kampuni ya kwanza nchini Tanzania kuzindua teknolojia ya 3G, 4G, na 4G+. Wateja wa Tigo mara zote wamekuwa ndio wa kwanza kutumia mtandao wenye kasi zaidi ambao hutokana na maendeleo na maboresho ya teknolojia.

Licha ya kuanza kwa mabadiliko haya ya kidijitali, wataalamu wametahadharisha uwepo wa changamoto mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi ambazo zinahatarisha viwango vya uwekezaji na ukuaji wake, jambo ambalo litaathiri huduma zitolewazo kwa wateja, biashara kwa ujumla na hata pato la serikali kutokana na sekta hii.

Moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikigusiwa zaidi ni ile wingi wa kampuni za mawasiliano katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania. Soko la Tanzania hivi sasa lina kampuni nane za mawasiliano ya simu. Wataalumu wa uchumi na teknolojia wanaeleza kuwa, kuimarisha soko itakuwa njia ya kuhakikisha sekta hii inakuwa bora na yenye tija zaidi na njia mojawapo muhimu ya kufanya hivyo ni kuunganisha japo kampuni mbili kati ya zilizopo sasa na kufanya kampuni chache kuwa na mtaji mkubwa zaidi, uwekezaji zaidi na ubora zaidi wa huduma ambao pia utashusha bei na kupandisha ubora. Moja ya kampuni ambazo zimechukua ushauri huu kwa vitendo na kuonyesha kusudio la kuungana ili kuboresha huduma na uwekezaji ni Tigo na Zantel. Kwa kuunganisha huduma, kampuni hizi zinaamini kuwa wateja kutoka kwenye kampuni hizo mbili wataweza kupata mtandaoa ambao ni imara na ulioenea zaidi, na pia watafurahia huduma zote ambazo zinatolewa na makampuni hayo, ikiwa ni pamoja na mtandao wa Tigo wa 4G na 4G+.
Hii itamaanisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wote, uwekezaji bora, gharama nafuu na pato zaidi kwa nchi yetu. Ni matumaini ya watumiaji wengi za simu za mkononi kuwa uimarishaji wa soko hilo kwa mbinu hizi na nyingine u karibu na utawapa nafuu na tija zaidi.

Send this to a friend