Uboreshaji wa sekta ya mawasiliano una mchango wa moja kwa moja kuikuza Tanzania ya Viwanda

0
16

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam

Tanzania ipo katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao umejikita katika kukuza viwanda kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mpango huo una malengo mawili, moja ni kuhakikisha ukuaji na mabadiliko ya kiuchumi na pili ni kupunguza umasikini.

Moja ya maeneo makuu ambayo mpango huo unaangazia ni maendeleo ya watu, na mabadiliko ya kijamii, ambapo mkazo umewekwa katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya, elimu na maendeleo ya ujuzi, akiba ya chakula pamoja na lishe bora.

Jambo la kuvuti zaidi ni kuwa teknolojia inachukua nafasi kubwa zaidi katika kushungulikia mambo mbalimbali ya malengo ya maendeleo, hasa katika suala la utoaji wa huduma muhimu.
Kwa mfano, teknolojia inatoa suluhisho katika utoaji wa huduma muhimu za afya. Ukuaji wa upatikanaji na unafuu wa utumiaji wa TEHAMA unasaidia kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma za afya kwa njia ya simu (m-health) mfano zoezi la usajili wa vizazi na vifo au bima za afya.

Tanzania ina uwiano wahuduma wa afya 5.1 katika kila kundi la watu 100,000. Hii ni asilimia 20 ya uwiano unaoshauriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Ukosefu wa huduma za afya huwaathiri zaidi watu wa hali ya chini, jambo ambalo huathiri maendeleo ya watu katika nchi kwa ujumla. Katika hali kama hii, huduma ya afya kwa njia ya simu ambayo inatolewa na makampuni ya mawasiliani nchini, inaweza kuwa ya msaada mkubwa sana.
Hivyo, ni vyema kama nchi tukaiunga mkono sekta ya teknolojia ya mawasiliano, na kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri kuweza kulinda huduma zao na kuhakikisha ukuaji wake.
Njia moja ya kuimarisha sekta hii ambayo imependekezwa na wataalamu wengi, ni kwenda katika soko lenye uimara zaidi. Ushahidi unaonesha kuwa hatua hii itasaidia kuimarisha sekta hiyo pamoja na kuhakikisha utoaji bora wa huduma kwa wateja, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya kwa njia ya simu kama nilivyoeleza hapo juu.

Kwa bahati nzuri, makampuni mawili, Tigo na Zantel yameonesha ni ya kuungana. Muungano huo utawezesha kupanua wigo wa utoaji wa huduma za afya kwa kutumia mtandao unganifu, kwani wateja wa kampuni hizo wataweza kutumia huduma za simu zinazotolewa na kampuni hizo.
Kwa mfano, wateja wa Zantel wataweza kufurahia huduma ya BIMA Mkononi. Hii ni huduma ya bima ya afya kupitia simu ya mkononi, bidhaa ambayo imezinduliwa karibuni na Tigo kwa kushirikiana na MILVIK Tanzania na Resolution Insurance ambayo hurejesha fedha kwa mteja kwa kila usiku atakaokuwa amelazwa hospitali. Huduma hii huzisaidia familia kukabili gharama za matibabu.
Kutokana na matokeo chanya ambayo yatapatikana endapo kukiwa na mtandao mkubwa na imara zaidi nchini Tanzania, suala la makampuni kuungana ili kuweka nguvu pamoja na kuboresha huduma kwa watumiaji ni la kupokelewa kwa mikono miwili.

Send this to a friend