Uchaguzi CHADEMA-Njombe wavurugika tena, wajumbe wakidaiwa si halali

0
48

Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliopangwa kufanyika leo Mjini Njombe umevurugika tena baada ya wanachama kudai kuwa wajumbe kutoka jimbo la Makete hawana uhalali wa kuwachagua viongozi.

Hii ni mara ya pili uchaguzi huo kufutwa baada ya uchaguzi wa awali kudaiwa kuwa haukufuata kanuni.

Mjumbe wa Kamati ya Sera, Ilani, Utafiti Kanda ya Nyasa, Dioniz Kipanya amesema uchaguzi huo umeshindwa kufanyika kutokana na mkanganyiko wa katiba unaosababishwa na hofu za kiuchaguzi, hivyo uchaguzi huo utafanyika na viongozi watapatikana.

“Hizi vurugu ambazo zimetokea ni mkanganyiko tu wa kikatiba ambao unasababishwa tu na hofu za kiuchaguzi, kwahiyo haya ni mambo ya kawaida katika chaguzi ni masuala tu ambayo tutayamaliza,” amesema.

Hapo awali, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Benson Kigaila aliwataka wapigakura hao kufuata kanuni za uchaguzi lakini hawakumsikiliza, na kuamua kuvunja mkutano.

Send this to a friend