Uchaguzi Kata ya Mzinga waahirishwa baada ya kifo cha mgombea

0
70

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesitisha uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Mzinga, Jimbo la Kivule, Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Chama cha Wananchi (CUF), Rashid Nandonde.

INEC imesema itapanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea, ambapo taratibu za uchaguzi wa udiwani katika kata husika zitaanza upya.

Hata hivyo, INEC imesema uteuxzi wa wagombea wengine ambao waluteuliwa kihalali utabaki kama ulivyokuwa awali, isipokuwa kama mgombea atajitoa na kwamba hakutakuwa na kampeni kwa wagombea Udiwani katika kata ya Mzinga mpaka baada ya uteuzi mwingine.

Send this to a friend