Uchaguzi Marekani: Donald Trump ajitangazia ushindi

0
55

Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amejitangazia ushindi licha ya kuwa bado mamilioni ya kura hayajahesabiwa.

Maafisa kadhaa wa chama hicho wameonesha kutokuunga mkono kauli hiyo ya Trump ambayo haina ushahidi wowote wa kuthibitisha ushindi wake.

Kiongozi huyo amesema kuwa atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Aliyekuwa Gavana wa New Jersey, Chris Christie amesema hatua hiyo ya Trump si sahihi kimkakati na si sahihi kutolewa na Rais.

Trump amekosoa utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya posta na kwamba umepelekea wizi wa kura, lakini hakutoa ushahidi wowote

Katika uchaguzi huo Rais Trump anachuana na aliyekuwa Makamu wa Rais katika utawala wa Barack Obama, Joe Biden.

Send this to a friend