Uchumi wa Tanzania wakua kwa 5.2% robo ya pili ya 2023

0
43

Uchumi wa Tanzania umeonyesha kukua kwa asilimia 5.2 katika robo ya pili ya mwaka 2023, ishara inayoonesha ahueni baada ya athari za janga la UVIKO-19 pamoja na vita vya Urusi na Ukraine.

Hii inathibitisha ukuaji chanya ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita, ambapo ulikua kwa asilimia 4.7 mwaka 2022 na asilimia 3.8 mwaka 2021.

Sekta zilizorekodi ukuaji mkubwa zaidi ni huduma za kifedha na bima, ambazo zilikuwa na ukuaji wa asilimia 15.6, ikifuatiwa na sekta ya umeme (asilimia 12.4), na sekta myingine ikiwemo burudani (asilimia 11.5).

Sekta ambazo zinaajiri watu wengi, kama vile kilimo, ujenzi, biashara na ukarabati, zilirekodi ukuaji wa wastani.

Mabilionea 10 wenye umri mdogo zaidi Afrika

Hata hivyo, kilimo kiliendelea kupungua kwa asilimia 2.4, ikionyesha kwamba licha ya ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini kunaweza kuendelea kusuasua kwa kuwa ukuaji unabaki katika sekta zinazowaajiri watu wachache.

Kwenye ripoti ya hivi karibuni ya mwenendo wa uchumi iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inaonesha kuwa uchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara utaendelea kupungua mwaka huu lakini unatarajiwa kuinuka tena mwaka 2024.

Ripoti hiyo inaangazia masuala kadhaa ambayo yameathiri uchumi wa Afrika mwaka huu, kama vile shinikizo la viwango vya ubadilishanaji wa fedha, mfumuko wa bei, na madeni.

Send this to a friend