Uchunguzi wa watoto njiti walionyofolewa macho na ulimi wabaini wauguzi walidanganya

0
53

Uchunguzi wa tukio la watoto njiti mapacha walionyofolewa macho, kuchunwa ngozi ya paji la uso na kukatwa ulimi katika kituo cha Afya Kaliua mkoani Tabora umebaini kuwa miili ya watoto hao ilitunzwa katika chumba cha wauguzi na si katika wodi ya wazazi kama ilivyosemwa awali na wauguzi hao.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Burian amesema baada ya uchunguzi huo, watumishi wanne wa kituo hicho cha afya waliohusishwa katika tukio hilo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mtoto wa miaka 14 ashtakiwa kwa kubaka mtoto mwenzie

Aidha, siku chache zilizopita katika mahojiano na CG FM ya Tabora, RC Batilda alisema baba wa watoto hao, Isaka Rafael amegoma kufanya mazishi ya watoto hao mpaka atakapokamatwa mtuhumiwa wa tukio hilo.

“Namuomba sana sana na nashukuru ndugu wa baba wote wanaunga mkono watoto wakazikwe naomba kijana wetu Isaka akubali kauli ya ndugu zake na sisi viongozi wa mkoa na wilaya, akubali twende tukawasitiri wale viumbe wa Mungu” alisisitiza.

Send this to a friend