Uchunguzi: Wanawake watumia vidonge 12 vya Flagyl kuzuia mimba

0
30

Madaktari bingwa wa masuala ya uzazi wametahadharisha matumizi ya kiwango kikubwa cha dawa aina ya Flagyl (metronidazole) kama njia ya kuzuia mimba kuwa hatari kwa afya kwani inaweza kuathiri utendaji kazi wa ubongo, uoni hafifu pamoja na kujenga usugu wa dawa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mkoani Dodoma na taasisi za elimu ya juu ambazo ni Chuo Kikuu cha St, John, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) umebaini kundi kubwa la wanawake kati ya umri wa miaka 18 hadi 45 wanatumia dawa hizo na baadhi wakitumia karibia vidonge 12 kwa siku jambo linalohatarisha afya.

Watafiti wamesema sababu za matumizi ya Flagyl kwa mujibu wa wahojiwa 470, asilimia 59 wamesema ni rahisi kuipata, asilimia 33 wanaona aibu kuulizia dawa nyingine ambazo ni rasmi kwa uzazi wa mpango, asilimia sita wamedai inapatikana kwa bei nafuu na asilimia mbili wamesema haina kiwango kikubwa cha hatari kama njia nyingine za uzazi.

Aidha, Daktari bingwa wa uzazi kutoka Idara ya Uzazi katika Hospitali ya Mwananyamala, Mugalu Kitandu amebainisha kuwa dawa hiyo ya antibaiotiki ikitumika isivyo, madhara yake ni kujenga usugu wa dawa, hivyo basi, badala ya kutibu ugonjwa husika kulingana na ushauri wa kitaalamu, aliyetumia dawa hizo kwa kiwango kikubwa hawezi kutibiwa kwa dawa za kawaida kwa kuwa mwili wake umejenga usugu wa dawa.

Poda ya watoto ya J&J yadaiwa kusababisha saratani

“Lakini dozi kubwa ya dawa hii inahusishwa na uvimbe, unaweza kupata saratani. Haya majibu yalitoka kwenye utafiti wa wanyama, kwa sababu dozi kubwa namna hiyo hazitakiwi kutumiwa na binadamu na hakuna utafiti uliothibitisha kwa binadamu, lakini ni muhimu kujitahadhari,” amesema mtaalamu.

Ameongeza kuwa kwa asilimia 70 Fragyl inaweza kusababisha mimba kutoka, yai likisharutubishwa ‘metronidazole’ linazuia lisikae kwenye ukuta wa kizazi.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend