UDART yatangaza kusitisha huduma za usafiri baadhi ya maeneo kutokana na mvua

0
5

Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, imepelekea kusitisha kwa muda kwa huduma za usafiri kwa uelekeo wa mabasi ya Mbezi/Kimara – Gerezani na Kivukoni.

UDART imesema imesalia na huduma za Mbezi/ Kimara – Magomeni Mapipa na Kimara kwenda Morocco, Mbezi, Mlonganzila na stendi ya Magufuli

Hatua hiyo ni baada ya mkondo wa maji wa Mto Msimbazi kuathiri matumizi ya Barabara katika eneo la Jangwani na kupelekea kufungwa kwa Barabara ya Magomeni Mapipa- Fire katika eneo la Daraja la Jangwani.

UDART imesema inaomba radhi kwa watumiaji wa usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na changamoto ya kujaa kwa maji katika eneo la Jangwani.