UDSM na UDOM vyakabiliwa na upungufu mkubwa wa wakufunzi

0
46

Ripoti iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni kuhusu utendaji wa jumla wa sekta ya elimu imebainisha kuwa baadhi ya vyuo vikuu nchini vinakabiliwa na upungufu wa wakufunzi, hali inayohatarisha utoaji wa elimu.

Kwa mujibu wa The Citizen, ripoti hiyo imeeleza kuwa vyuo vilivyoathirika zaidi ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambacho kinakabiliwa na upungufu wa wakufunzi 2,479 pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinachokabiliwa na upungufu wa wakufunzi 856.

Hata hivyo, kuna wasiwasi kuwa upungufu huo unaweza kuathiri vibaya mchakato wa masomo kwa kuwa idadi kubwa ya wakufunzi wanaokosekana ni wa upande wa taaluma.

Send this to a friend