Ufafanuzi wa Bodi ya Filamu kuhusu taarifa ya tozo za kutengeneza maudhui ya video

0
23

Bodi ya Filamu Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuhusu tozo za huduma mbalimbali zinazodaiwa kutolewa na bodi hiyo.

Bodi hiyo imesema kuwa imesikitishwa na usambaaji wa taarifa hizo kwa kuwa si za kweli na hazina usahihi wowote na kwamba zinalenga kuzua taharuki na kuupotosha umma kuhusu utoaji wa huduma za bodi.

Aidha, bodi hiyo imesema kuwa Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza za Juni 2020 zilitokana na maoni ya wadau ambayo yalipelekea kushushwa kwa tozo zilizokuwa katika kanuni za mwaka 2011 tofauti na taarifa inayosambazwa.

Kufuatia hali hiyo, mamlaka hiyo imesema haitosita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote atakayehusika na kusambaza taarifa hizo.

Send this to a friend