Ufafanuzi wa JKT vijana 147 waliobainika na maambukizi ya VVU

0
43

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema idadi ya vijana 147 waliogundulika kupata maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kambini walipata ugonjwa huo wakiwa nje ya makambi.

Akitoa ufafanuzi huo Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kupitia taarifa ya Kamati ya Bunge inayohusiana na masuala ya UKIMWI iliyotolewa Februari 03, 2022 bungeni Dodoma imezua taswira mbaya kuwa vijana hao wamepata maambuki hayo wakiwa ndani ya makambi ya jeshi jambo ambalo si sahihi.

Hospitali ya Bugando yaanza utafiti kuhusu maji ya maiti kutumika kuhifadhia samaki

Brigedia Mabena amedai vijana wanaomaliza kidato cha sita na kujiunga na jeshi hilo hupimwa VVU wanapowasili kwenye makambi ya jeshi, ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi 2020/2021 idadi ya vijana 147 waliogundulika walipata maambukizi kutoka sehemu mbalimbali.

“Katika kupima afya ndiyo ile idadi ambayo iliweza kutolewa taarifa yake bungeni ndio walibainika, na baada ya sisi JKT kuwabaini kwamba wamepata maambukizi kuna wengine ‘wanapanic’. Kupitia wataalamu wetu wa saikolojia walioko katika makambi yetu wamekuwa wakiwapa ushauri nasaha. Kwa hiyo hao vijana wameendelea kutibiwa, na wale ambao wamebainika wamefikia hatua ya kupewa dawa waalinza kupewa dawa,” ameeleza Brigedia Mabena.