Ufafanuzi wa Polisi kuhusu vijana wa CCM kukamatwa kwa tuhuma za kutaka kuchoma nyumba ya Mbunge

0
38

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limetoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vijana sita wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukamatwa nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Kenan wakiwa na petroli lita 20 kwa lengo la kuiangamiza familia ya mbunge huyo.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, imesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa vijana hao waliokamatwa na wafuasi wa CHADEMA walifika nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali majira ya saa moja jioni wakiwa na pikipiki mbili na dumu lenye mafuta ya petroli lita 20 kwa lengo la kuchukua pikipiki zingine zilizokuwa hapo na kuziwekea mafuta.

“Kwa kuwa nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya na nyumbani kwa Mbunge ni karibu sana nyumba zao zikitenganishwa na barabara, ndipo vijana hao walipokamatwa na kutuhumiwa kwamba walikuwa na lengo la kuchoma moto nyumba ya Mbunge Aida,” imeeleza taarifa ya Polisi.

Send this to a friend