Ufafanuzi wa Polisi video ya askari aliyechukua fedha kwa raia wa kigeni

0
55

Baada ya kusambaa kwa video fupi katika mitandao ya kijamii ikimuonesha askari Polisi akichukua fedha kwa raia wa kigeni baada ya mazungumzo, Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi juu ya askari huyo pamoja na hatua zilizochukuliwa.

Akitoa ufafanuzi huo leo Septemba 14, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema inawezekana wanao isambaza video hiyo hawakupata mrejesho wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari huyo aliyeendekeza tamaa zake binafsi na kuifedhehesha Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla.

IGP Wambura afanya mabadiliko Makamanda wa Polisi

Misime amebainisha kuwa “ni kweli tukio hilo lilitokea huko katika Mkoa wa Kaskazini Unguja miaka mitano iliyopita ambapo askari huyo alishtakiwa na ndani ya siku tatu alipatikana na hatia na kufukuzwa kazi kwa fedheha ili iwe fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo.”

Sambamba na hilo Misime amewahakikishia watanzania kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali askari yeyote atayekiuka kiapo chake na kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.

Send this to a friend