Ufafanuzi wa serikali kuhusu kidato cha sita kwenda shule na malimao na tangawizi

0
53

Serikali imekanusha taarifa kuwa imewataka wanafunzi wa kidato cha sita watakaoanza masomo Juni Mosi mwaka huu kwenda shuleni wakiwa na malimao na tangiwizi.

Kanusho hilo limekuja siku chache kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa baadhi ya shule za bweni zimewataka wanafunzi kubeba malimao na tangiwizi, huku shule nyingine zikidaiwa kuwataka wanafunzi kulipa fedha kwa ajili ya bidhaa hizo kama kinga dhidi ya virusi vya corona.

Hivi karibuni Shule ya Sekondari St. Mary’s-Mazinde Juu ilikanusha taarifa kuwa imewataka wanafunzi wa kidato cha sita kulipa TZS 750,000 kwa ajili ya kununua malimao na tangawizi.

Hata hivyo, siku chache zilizopita Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara alisema kuwa si vibaya wanafunzi wakibeba tangawizi, malimao na hata wakiamua kujifukiza wawapo shuleni.

Wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanajiandaa na mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari utakaoanza Juni 29 mwaka huu wanatarajiwa kuanza masomo Juni 1, 2020, lakini wanafunzi wa madarasa mengine wataendelea kusalia majumbani.

Send this to a friend