Ufafanuzi wa Serikali kuhusu kutotangaza shule bora kidato cha nne
Waziri wa Elimu, Adolf Mkenda amesema uamuzi wa kutotangaza shule na wanafunzi bora katika matokeo ya mwisho ya mtihani ni kutokana na utata wa namna ya kuzitathmini shule na wanafunzi hao.
Akitoa ufafanuzi huo Bungeni amesema uamuzi huo ulifikiwa mwezi Novemba kwenye kikao cha Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ambapo baraza halikutangaza shule bora katika matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa Desemba 1, 2022 pamoja na matokeo ya kidato cha nne mwaka huu.
Aidha, Waziri Mkenda amefafanua kuwa takwimu zote ambazo zinaonesha shule zilizopata alama za juu na shule zilizopata alama za chini zote ziko hadharani.
Zaidi msikilize hapa chini akitoa ufafanuzi huo bungenI;