Ufafanuzi wa TFF kuhusu usajili wachezaji wa kigeni

0
41

Kutokana na sintofahamu inayoendelea baada ya Klabu ya Yanga kuzuiwa usajili wa mchezaji Tuisila Kisinda na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Shirikisho limesema Klabu kujaribu kusajili wachezaji wa kigeni zaidi ya 12 ni kwenda kinyume na sheria.

“Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12, hivyo Klabu kutaka au kujaribu kusajili wachezaji zaidi ya idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni,” imesema TFF.

TFF yamzuia Kisinda Yanga

TFF imesema usajili wa wachezaji wa kigeni hasa kwa Klabu ambazo timu zao zinacheza mashindano ya kimataifa ulishapitishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF, ambapo katika mazingira maalum ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao ili wawahi usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Imeongeza kuwa wachezaji wote wa Klabu hizo za Azam, Geita Gold, Simba na Yanga walishapewa leseni zao kwaajili ya msimu wa 2022/2023 ambazo pia ndizo zimetumika kuwaombea usajili kwaajili ya mashindano ya CAF.

Send this to a friend