Ufaransa inapambana kudhibiti kunguni kabla mashindano ya Olimpiki mwakani

0
45

Wakati Michezo ya Olimpiki ya Paris ikikaribia kufanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, mamlaka nchini Ufaransa wanafanya kila liwezekanalo kuwadhibiti wadudu aina ya kunguni ili kuepusha aibu na usumbufu unaoweza kutokea wakati wa tukio hilo.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakichapisha video za wadudu hao ambao huonekana kwenye treni za kasi na vituo mbalimbali mjini Paris, na makala nyingi zimeandikwa mitandaoni zikizungumzia uwepo wa wadudu hao na zingine zikioneshwa kwenye wavuti katika sinema na hata uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle.

“Serikali inahitaji haraka kuweka mpango wa hatua dhidi ya janga hili kwa sababu Ufaransa inajiandaa kuandaa Michezo ya Olimpiki na Paralympic mwaka 2024,” Naibu Meya, Emmanuel Gregoire, alisema kwenye barua kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne wiki hii.

Adanganya ametekwa ili apate muda wa kukaa na mchepuko

Waziri wa Uchukuzi, Clement Beaune pia ameahidi kujadili suala hilo na wahudumu wa usafiri wiki ijayo, lengo likiwa kushughulikia tatizo kwa vitendo na kuzuia aibu au usumbufu unaoweza kutokea.

Ripoti iliyochapishwa na shirika la afya la Anses mwezi Julai, ilionyesha kuwa kati ya mwaka 2017 na 2022, kunguni walienea zaidi ya kaya moja kati ya 10 nchini Ufaransa. Kuenea kwa wadudu hao kumesababisha taharuki kati ya watu, na baadhi kuwa na wasiwasi juu ya suala hilo.

Send this to a friend