Ufaransa yafunga shule kutokana na kunguni

0
56

Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Gabriel Attal ametangaza siku ya Ijumaa kuwa nchi hiyo imelazimika kufunga shule saba baada ya kuvamiwa na kunguni ambao wametapakaa kila mahali.

Mapema wiki hii, mamlaka ya Paris ilitangaza kufungwa kwa shule mbili kwa sababu ya kunguni, moja huko Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Waziri wa Usafirishaji alikutana na makampuni ya usafirishaji wiki hii kubuni namna ya kufuatilia na kunyunyizia dawa katika vyombo vya usafiri wa umma na kujaribu kupunguza wasiwasi nchini humo uliochochewa zaidi na vyombo vya habari.

Nyota wa MTV afariki baada ya kufanya ‘plastic surgery’

Baada ya taarifa kuwa kunguni walipatikana kwenye jengo la sinema mwezi mmoja uliopita, raia wa Ufaransa walianza kusambaza video katika mitandao ya kijamii zikionesha wadudu hao wakitambaa majumbani na kwenye usafiri wa umma kama matreni na mabasi.

Kunguni wamekuwepo Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya kwa miongo kadhaa. Mtaalamu wa vidudu kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Mediterenia mjini Marseille, Ufaransa, Jean-Michel Berenger, anasisitiza kuwa kunguni hawatokani na uchafu, bali wanachofuata ni damu ya mtu.