Ufaransa yapiga marufuku iPhone 12

0
13

Mamlaka nchini Ufaransa imeagiza kampuni ya teknolojia ya Apple kuacha kuuza simu ya iPhone 12 kutokana na viwango vya mionzi kuwa juu ya kiwango kinachokubalika kisheria.

Waziri wa Dijitali wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, ameliambia gazeti la Ufaransa la Le Parisien kuwa ikiwa Apple haitaweza kutatua tatizo hilo, italazimika kurejesha kila iPhone 12 iliyowahi kuuzwa nchini humo.

“Apple inatarajiwa kutoa majibu ndani ya wiki mbili. Ikiwa hawatofanya hivyo, nipo tayari kutoa amri ya kurudisha iPhones zote za aina ya 12 zilizoko sokoni. Sheria ni ile ile kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa ya kidijitali,” amesema.

BoT: Unaporudishiwa fedha chakavu usikatae

Aidha, Apple imeiambia BBC kuwa inapinga tamko hilo la Wakala wa Kitaifa wa Masafa (ANFR) na kusema kwamba bidhaa hiyo imeidhinishwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa kuwa inakidhi viwango vya kimataifa vya mionzi.

Send this to a friend