Uganda: Amkata vipande mpwa wake na kumpa mkewe apike

0
43

Polisi nchini Uganda wanamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 34 kwa kumkata vipande vipande mpwa wake mwenye umri wa miaka tisa kisha kuweka sehemu ya mwili wake kwenye sufuria na kumpa mke wake ili apike.

Ripoti zinaeleza kuwa siku ya Jumapili mke wa mshukiwa alipogundua kuwa mumewe alikuwa amempa vipande vya binadamu kupika aliita msaada ambapo wakazi wa eneo hilo walifika na kumtambua marehemu mvulana wa miaka tisa ambaye ni mtoto wa kaka mkubwa wa mshukiwa.

Diwani wa Kaunti Ndogo ya Rubaare, John Kabeho ameliambia gazeti la Monitor kuwa mshukiwa alimuua mpwa wake wakati mkewe hayupo nyumbani.

Amchoma kisu aliyekuwa mkewe pamoja na mpenzi wake mpya

“Mshukiwa alibaki nyumbani na mtoto huyo wakati mkewe na mtoto wao wakiwa wameenda kanisani. Mkewe aliporudi kanisani, mumewe alimwambia amenunua nyama na ilikuwa kwenye sufuria jikoni. Alimwagiza mkewe aipike haraka kwa sababu alikuwa na njaa,” amesema Kabeho.

Ameongeza kuwa mshukiwa huyo alianza kuwa na matatizo ya akili mwaka 2020 na alifikishwa hospitalini akawa mzima na kurejea nyumbani. Hata hivyo, aliendelea kuonyesha dalili za matatizo ya kiakili na kupelekwa kanisani kwa ajili ya maombi ambapo wanafamilia wanasema alikuwa amepata nafuu.

Send this to a friend