Uganda: Idadi ya wanaume wanaopima DNA yaongezeka baada ya kuhisi watoto si wao

0
10

Uganda imekumbwa na wimbi jipya la wanaume ambao hali yao imewafanya kufika kwa wingi katika ofisi ya Wizara ya Masuala ya Ndani ya Nchi wakitaka hati za kusafiria za watoto wao zifutiliwe mbali baada ya vipimo vya DNA kubaini kuwa hawakuwa baba zao halisi.

Kurugenzi ya Udhibiti wa Uraia na Uhamiaji ya Uganda (DCIC) tayari imepokea barua kutoka kwa wanaume wasiopungua 32 wanaotaka hati za kusafiria za watoto wao zifutwe baada ya matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba wao si baba wa kuwazaa, na kutaka maelezo yao yatolewe kwenye pasipoti za watoto hao.

Balaa zima lilitokana na raia wa Uganda mwenye makazi yake Ulaya alipogombana na mkewe ambaye kwa bahati mbaya alitamka kuwa yeye si baba halisi wa watoto wao, hivyo aliamua kuchukua sampuli za DNA kwa ajili ya kupima kwa siri na kwa mshangao mkubwa alishtuka baada ya kujua kuwa ni kweli hakuwa baba wa mtoto yeyote kati ya wale sita.

Akamatwa kwa madai ya kuponya UKIMWI kwa kitunguu

Mwanamume huyo, ambaye alikuwa akiwasomesha watoto wote sita katika shule za bei ghali nje ya nchi, hakuridhika na matokeo ya awali na ndipo alipochukua baadhi ya sampuli kwenda Canada na nyingine Afrika Kusini na wote walithibitisha kitu kimoja kuwa hakuna mtoto wake hata mmoja kati ya sita.

Hili lilichochea ongezeko kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa katika vipimo vya DNA nchini Uganda huku idadi ya wanaume wanaotafuta vipimo vya DNA ya uzazi kwa watoto wao ikiongezeka kwa asilimia 70.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uganda imesema wastani wa idadi ya wanaume waliotaka kupima uzazi miaka mitatu iliyopita ilikuwa watatu kwa mwezi lakini kwa kiasi kikubwa imepanda hadi mia moja kwa muda huo huo.