Uganda kukopa bilioni 500 kufidia kampuni ya umeme baada ya mkataba kumalizika

0
21

Bunge la Uganda limeidhinisha ombi la serikali la kukopa dola milioni 190 [TZS bilioni 502.5] kutoka Benki ya Stanbic ili kufidia kampuni ya usambazaji umeme, Umeme Limited, kwa pesa ambazo hazijarejeshwa baada ya kampuni hiyo kuwekeza katika miradi ya umeme.

“Bunge limeidhinisha ombi letu kama serikali la kukopa dola milioni 190 kutoka Benki ya Stanbic kwa ajili ya fidia ya Umeme,” Waziri wa Nishati, Ruth Nankabirwa aliandika kwenye jukwaa la kijamii X.

Serikali ya Uganda imeamua kutoendelea na makubaliano na kampuni hiyo ya umeme baada ya mkataba wake kumalizika.

Hata hivyo, kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo, serikali inapaswa kufidia kampuni hiyo ya Umeme kwa uwekezaji wowote wa mtaji katika mtandao wa usambazaji umeme ambao kampuni hiyo haijaupata kufikia mwisho wa kipindi cha mkataba.

Send this to a friend