Uganda kumrejesha Tanzania Mtanzania aliyekutwa na corona

0
27

Wizara ya Afya ya Uganda imesema kuwa itamrejesha nchini Tanzania Mtanzania aliyebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo katika mpaka wa Mutukula.

Aprili 17 wizara hiyo ilithibitisha kisa kimoja ambapo taarifa ya awali ilieleza kuwa maambukizi hayo yametokea miongoni mwa jamii nchini humo, taarifa ambayo baadae ilikanushwa kuwa haikuwa sahihi.

Katika taarifa mpya wizara hiyo imesema aliyebainika kuwa na maambukizi hayo ni dereva wa lori mwenye miaka 34 ambaye ni raia wa Tanzania, na aliwasili Mutukula Aprili 16 akitokea jijini Dar es Salaam.

Dereva huyo hakuwa na dalili yoyote yenye kuonesha kuwa alikuwa na maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19), na sasa jitihada za kumtafuta na kurejesha nchini Tanzania zinaendelea, wizara imesema.

Kutokana na msahihisho hayo, visa vya watu wenye maambukizi ya COVID-19 nchini Uganda vinabaki kuwa 55.

Send this to a friend