Serikali ya Uganda na kampuni ya Vitol Bahrain E.C. yenye makazi yake Bahrain, wamechagua bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuagiza mafuta kama sehemu ya jitihada za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Uganda.
Uamuzi huo ulifanywa siku chache baada ya Vitol Bahrain E.C. kupata kibali kutoka Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) kusambaza mafuta nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti, Uganda ambayo kwa sasa inaagiza asilimia 90 ya mafuta yake kupitia Kenya, haikuwa na habari kuhusu mazungumzo yanayohusu makubaliano kati ya serikali ya Kenya na mataifa mawili ya Ghuba (Saudi Arabia na UAE) na hivyo kukasirishwa kwa sababu Uganda ilikuwa ikitegemea sana usambazaji wa mafuta kutoka Kenya.
Israel kuongeza jitihada kuwapata Watanzania waliotekwa na Hamas
Katika mikutano iliyofanyika wiki iliyopita, wawakilishi wa Wizara ya Nishati ya Uganda, Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC), na wauzaji wa mafuta wa Kenya walibaini kuwa uamuzi wa Kenya kuingia kwenye makubaliano na Ghuba uliacha usambazaji wa mafuta wa Uganda kuwa hatarini na kuwafanya raia wake kukumbana na bei kubwa ya mafuta.
“Ili kuhakikisha usalama wa usambazaji, ushirikiano huu unahakikisha kuwa kutakuwa na akiba ya kutosha nchini Uganda na Tanzania ambayo itatumika ikiwa kutakuwa na usumbufu wa usambazaji nchini,” Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Ruth Nankabirwa