Uganda: Waziri asema maskini hawatakwenda mbinguni sababu ya malalamiko

0
40

“Watu maskini hawatakwenda mbinguni kwa sabbabu wanamtusi Mungu kupitia malalamiko na shutuma zao kila siku,” amenukuliwa mwanasiasa mwandamizi wa Uganda akisema.

Gazeti la New Vision la Uganda limeeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kahinda Otafiire ametoa matamshi hayo kwenye hafla ya shule iliyoko Magharibi mwa nchi hiyo akiwaambia wanafunzi kuwa, kufanya kazi kwa bidii ndio mwarobaini wa umaskini.

Ameonesha kushangazwa na baadhi ya watu ambao hawataki kufanya kazi lakini wanataka kuwa matajiri.

“Usipotumia zana ambazo Mungu amekupa, usimlaumu unapokuwa maskini. Pambana kujikwamua kwenye umaskini kwa sababu kuwa tajiri ni fahari,” amenukuliwa akitoa maelezo hayo.

Uganda kama mataifa mengine duniani inakabiliwa na tatizo la ajira hasa kwa vijana, ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya vijana, ambapo asilimia 75 ya raia wake wapo chini ya umri wa miaka 30.

Send this to a friend