
Jeshi la Polisi nchini Uganda limekanusha kuwashikilia wanaharakati wawili wa Kenya wanaodaiwa kutekwa nyara siku ya Jumatano katika mji mkuu Kampala.
Mwanasiasa mkuu wa upinzani, Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ alisema wawili hao, Bob Nyagi na Nicholas Ayoo walitekwa nyara na kupelekwa kusikojulikana na watu aliowaita maafisa usalama ambao hawakuwa na sare, wakiwa kwenye kituo cha mafuta.
Bob na Nicholas walikuwa wameshiriki hivi karibuni katika mikutano ya kampeni ya Bobi Wine, ambaye anatafuta kumng’oa Rais aliye madarakani, Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa takribani miongo minne.








