Uganda yapinga sheria ya kufanya chanjo kuwa lazima

0
47

Sheria mpya iliyopendekezwa nchini Uganda ya kufanya chanjo kuwa ya lazima kwa watu wazima wote endapo kutatokea mlipuko wa ugonjwa mkubwa, imekataliwa na bunge la Uganda.

Wizara ya afya imesema, mswada huo uliundwa kukabiliana na athari za kiafya na magonjwa yanayoibuka kama vile homa ya kuvuja damu (haemorrhagic fevers) , na ilipendekeza watakaovunja sheria yoyote kutozwa faini ya hadi $1,045 (TZS milioni 2.4) au wakabiliwe na kifungo cha miezi sita jela.

Lakini wabunge waliibua mjadala kuhusu haki za watu kuchagua, na kuhoji ni nani atawajibika endapo kutatokea madhara yoyote ya chanjo.

Uganda kwa sasa inakadiriwa kufikia lengo lake la kutoa chanjo kwa watu milioni 22 ikiwa ni nusu ya wakazi wake dhidi ya Covid-19.

Nchini Uganda chanjo ya mara kwa mara kwa watoto dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, bado ni ya lazima isipokuwa katika magonjwa mapya ya mlipuko yanayoibuka.

Send this to a friend