Ugonjwa usiojulikana waua 12 Uganda

0
39

Wataalamu wa afya nchini Uganda wanachunguza mlipuko wa ugonjwa usiojulikana ambao umeua takribani watu 12 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika wilaya ya Kyotera iliyoko katikati mwa Uganda.

Waathirika wa ugonjwa huo hutokwa na vipele mwilini ambavyo vinasambaa na kuwa vidonda na kisha kuumwa kwa siku chache kabla ya kufariki dunia huku wengine wakionesha dalili za kuvimba baadhi ya viungo vya mwili.

Wizara ya afya nchini humo imesema sampuli ya ngozi ya mmoja wa wagonjwa aliyefariki imechukuliwa ili kufanyia vipimo, ambapo matokeo ya sambuli hiyo bado hayajatangazwa kwa umma.

Serikali: Mjamzito akifariki kwa uzembe, Mganga Mkuu wa Mkoa, Wilaya ni watuhumiwa

Aidha, maafisa wa afya wa eneo hilo wameeleza kuwa imekuwa vigumu kudhibiti hali hiyo kwani baadhi ya wagonjwa wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji badala ya kwenda hospitali.

Send this to a friend