Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linafanya kazi na wataalamu kuibua jina jipya la ugonjwa wa homa ya nyani ‘Monkeypox’ ili kuepusha ubaguzi.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanasayansi zaidi ya 30 wiki iliyopita kuandika kuhusu haja ya dharura ya jina lisilobagua na lisilonyanyapaa la virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa huo.
Aidha, wameeleza kuwa kuendelea kufananisha virusi hivyo kama Mwafrika sio sahihi na ni ubaguzi.
Shirika hilo linasema watu zaidi ya 1,000 wameambukizwa virusi vya homa ya nyani katika mlipuko wa sasa hasa katika mataifa ya Magharibi.