Uhalifu nchini waongezeka kwa asilimia 5.2

0
40

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni amesema katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 makosa makubwa ya uhalifu yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi yameongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2020/21.

Ameeleza hayo wakati akiwasilisha bungeni Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/2023,  ambapo amesema mwaka 2021/22 idadi ya makosa yaliyoripotiwa ni 39,182, huku 2020/2021 makosa yaliyoripotiwa yakiwa ni 37,250.

Aidha katika ripoti yake amesema kati ya makosa yaliyoripotiwa, upelelezi wa kesi 15,339 ulikamilika na watuhumiwa 16,514 walifikishwa mahakamani. Kati ya kesi hizo 2,673 zilishinda, kesi 388 zilishindwa na kesi 12,278 zinaendelea kusikilizwa mahakamani.

Waziri Ameongeza kuwa 2022/23 Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa kesi zote zinafanyiwa kazi kwa haraka ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend