Uhamiaji: Tumewatambua wanaohujumu uwekaji mipaka Loliondo

0
44

Idara ya Uhamiaji imesema wamewatambua watu ambao wamehusika na hujumu katika zoezi la uwekaji wa mikapa katika Pori Tengefu la Loliondo mkoani Arusha.

Kamishina wa Uhamiaji anayehusika na udhibiti wa mipaka Tanzania, CI Samwel Mahirane amesema Uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wameanza uchunguzi wa watu waliotajwa kuhujumu zoezi, kujua kama ni raia wa Tanzania ama si Watanzania hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Muda wowote kuanzia sasa tutawakamata na kama ni Watanzania wamekwenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu hatua sitaiki zitachukuliwa dhidi yao,” amesema.

Pia amesema kama kuna Mtanzania aliyeujumu zoezi hilo na akakimbilia nchi jirani ni  vyema akajitokeza vinginevyo watawakamata kwa sababu taarifa wanazo taarifa.

Aidha, amesema asasi za kiraia ambazo zinafanya kazi katika wilaya ya Ngorongoro na  Tanzania ambazo zilijisajili kwa lengo la kusaidia jamii zinakwenda kuchunguzwa upya ili kubaini uhalisia wa kazi wanazofanya kama alivyoelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mhandisi Hamad Masauni.

Send this to a friend