Uhamiaji yakanusha Watanzania kunyang’anywa pasipoti Airport

0
63

Idara ya Uhamiaji imekanusha taarifa kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi wanaporejea nchini wananyang’anywa pasipoti, pesa na kuhojiwa.

Taarifa iliyotolewa leo na Idara ya Uhamiaji imeeleza kuwa taarifa hiyo ina lengo la kupotosha umma na kuleta taharuki kwenye jamii.

“Taarifa hizo ni za uzushi zenye lengo la kupotosha umma na kuleta taharuki kwa jamii. Hivyo Watanzania wanapaswa kuzipuuza,” imesema taarifa hiyo.

Send this to a friend