Uingereza kuleta wawekezaji wa biashara na utalii nchini Tanzania

0
35

Serikali ya Uingereza imesema itawashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania baada ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania.

Ahadi hiyo imetolewa na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza (Boris Johnson) katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania, Lord John Walney alipofanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Scotland.

Walney amekutana na Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Rais Samia amesema Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

 

Send this to a friend