Ujenzi Mwendokasi Posta-Boko kuanza Oktoba 15

0
12

Ujenzi wa miundombinu ya kupita mabasi yaendayo haraka (DART) kupitia Barabara ya Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi na Sam Nujoma unatarajia kuanza Oktoba 15, mwaka huu.

Akizungumza Kaimu Meneja wa Mipango ya Usafirishaji DART, Mhandisi Mohammed Kuganda amesema ujenzi huo ni wa mradi wa mabasi yaendayo haraka awamu ya nne ambao utaanzia maeneo ya Maktaba Kuu, Barabara ya Bibi Titi kupitia Mwenge na kisha Mawasiliano ambayo itaenda kukutana na daraja la Ubungo.

Ameongeza kuwa ujenzi mwingine utaanzia Mwenge kuelekea Boko (DAWASA) ambapo ujenzi wa Barabara zote zinatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 400 zikiwa na urefu wa kilometa 30.1 na kila barabara itakuwa na mkandarasi wake.

Akizungumzia kuhusu upanuzi wa kituo cha Kivukoni, Kuganda amesena ujenzi utaanza Oktoba 21, mwaka huu baada ya kituo cha daladala kuhamishwa ambapo kituo hicho kitakwenda kuhudumia zaidi ya mabasi ya mwendokasi 3,200 pindi awamu zote zitakapokamilika.

Wafungwa 691 wanasubiri adhabu ya kifo nchini

Aidha, DART imefafanua kuwa kuondolewa kwa kituo cha daladala kutazihusisha dalala zilizokuwa zikifanya safari zake maeneo mbalimbali na kuishia kituo hicho, na mwisho wa kutumia eneo hilo ni Oktoba 20 ambapo zimepewa maeneo mengine ya kumalizia safari zao.

Send this to a friend