Ujenzi wa madarasa na vituo vya afya wawanufaisha mafundi wazawa

0
46

Ilizoeleka kwamba miradi inayotokea kwenye maeneo mbalimbali nchini tenda ilikuwa ikipewa kwa mafundi na wakandarasi kutoka nje lakini hali imekuwa tofauti Mkoani Mtwara  baada ya mafundi wazawa kupewa kazi ya kujenga kituo afya wilaya ya Nanyumbu.

Haji Hamisi ni fundi aliyeshiriki ujenzi wa kituo hicho cha afya aneleza kwamba fursa waliyopewa na serikali ya wamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu ni nzuri kwani inawasaidia kiuchumi kwa kuweza kumnufaisha yeye pamoja na mafundi wengine.

“Kwanza huu mradi umetunufaisha au umeninufaisha mimi pamoja na mafundi ambao nimewaajiri kwa sababu huu mradi sasa hivi imefikia mimi kuna mafundi kama 22 ambao nafanya nao kazi hapa na wanapata hela na kuendesha maisha yao.

Binafsi nasema huu mradi unaninufaisha na mimi mwenyewe kwenye katika ufundi maana yake nazidi kuonyesha kazi yangu kwa ubora. Kama serikali itaendelea kutupa miradi kama hii maana yake sisi tutatoka katika hatua moja kwenda nyingine,” alisema Hamisi.

Send this to a friend