Ujenzi wa Mwendokasi Gongolamboto kuanza

0
72

Kaimu Meneja wa Mipango na Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Mohamed Kuganda amesema ujenzi wa miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka ‘Mwendokasi’ awamu ya tatu unatarajia kuanza.

Akizungumza na Habari Leo amesema taratibu zote ikiwa ni pamoja na mkandarasi kuoneshwa eneo la kazi zimekamilika ambapo zoezi hilo limefanyika juzi jijini Dar es salaam.

Amesema mradi huo ambao utakaoanzia katika barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha mwendokasi cha Posta ya zamani hadi Gongolamboto, utajumuisha tawi la kutokea daraja la Mfugale katika barabara ya Mandela hadi Buguruni, kupitia barabara ya Uhuru hadi Gerezani kupitia barabaraa za Shaurimoyo na Lindi.

Kuganda amesema, mpaka kukamilika kwa mradi huo utagharimu TZS bilioni 231 pamoja na VAT kwa Lot 1 ikiwa ni gharama za ujenzi wa barabara huku lot 2 inayohusu majengo bado haijajulikana gharama zake kwa kuwa mkandarasi hajapatikana.

Mradi huo utachukua muda wa miezi 36 kutoka sasa na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2025.

Send this to a friend