Kaya 12 zenye mashamba katika mtaa wa Bulengahasi mji mdogo Katoro wilayani Geita zimeulalamikia uongozi wa kitongoji na kata kwa madai ya kutowapa taarifa za kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi wa shule ya sekondari katika mashamba yao ambapo tayari walikuwa wameshapanda mazao.
Wananchi hao wamesema utekelezaji wa ujenzi wa shule hiyo umesababisha kuharibu mazao yao hasa mahindi, kitendo ambacho wamekilalamikia kwani wamedai hapakuwa na ushirikishwaji wa jambo hilo kwa baadhi ya wamiliki wa mashamba hayo.
Mchungaji kortini kwa tuhuma za kutapeli bilioni 1.6
Wamefika katika eneo la mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari baada ya kupata taarifa za uharibifu wa mazao yao bila kushirikishwa hali ambayo imeleta sintofahamu. Wamesema mradi huo wanaupokea kwani waliuhitaji muda mrefu wanaomba taratibu za tathimini za kuwatambua zifanyike ili ujenzi wa mradi huo uendelee.
Mtendaji wa kata ya Katoro, Seleman Mahushi wakati akijibu malalamiko ya wananchi hao amesema wananchi wote walipewa taarifa juu ya mradi huo na wakakubali kubadilishiwa maeneo ili kupisha ujenzi wa mradi huo.