Ujumbe wa Dkt. Shoo kwa Wakristo kuhusu chanjo ya UVIKO19

0
28

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofy Dkt. Frederick Shoo amesisitiza kuwa chanjo inayotolewa kudhibiti athari za maambukizi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19) haina uhusiano wowote na mpinga Kristo wala alama ya 666 iliyoandikwa kwenye kitabu cha ufunuo 13.

Rais Samia alivyombana Askofu Gwajima hadharani chanjo ya Corona

“Hao wanaosema hivyo hawaelewi kabisa maandiko matakatifu sawasawa. Kwa mtu aliyesoma historia ya kanisa, historia ya maandiko matakatifu anaelewa kabisa kuwa hayana uhusiano na mwisho wa dunia wala jambo hilo la UVIKO19,” amesisitiza Dkt. Shoo.

Ifahamu mikoa inayoongoza Tanzania kwa kutoa chanjo ya UVIKO19

Amesema watu wasio na uelewa ndio wanadanganya wengine kuhusu chanjo hiyo, hivyo viongozi wa dini wana wajibu wa kuendelea kuelemisha waumini wao ili kukabili janga la UVIKO19.

Mambo ya kufahamu kuhusu chanjo ya Sinopharm inayoletwa nchini kutoka China

Kwa upande wake Askofu Gervas Nyaisonga kutoka Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) amesema kuwa ili kukabiliana na ugonjwa huo, kanisa hilo limeacha baadhi ya taratibu ikiwemo kuchovya maji ya baraka, badala yake katika baadhi ya maeneo wanatumia yanayotiririka.

Viongozi hao wameongeza kuwa chanjo hiyo ni sehemu ya kawaida kabisa kama zilivyo chanjo nyingine za kifaduro, pepopunda na kifua kikuu, na kwamba tofauti ni hiyo ya UVIKO inatolewa kwa watu wazima.

Viongozi wamshukia Askofu Gwajima sakata la chanjo

Hadi Oktoba Mosi mwaka huu zaidi ya Watanzania 500,000 tayari wamechanjwa, huku mikoa ya Katavi, Lindi na Mtwara ikiongoza kwa kuchoma wananchi wengi zaidi.

Send this to a friend