Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema sheria zinazowaelekeza TFF kufungia watu zimetengenezwa na viongozi waliopita na hazikusainiwa na yeye.
Akizungumza wakati wa kufunga semina ya siku moja ya waandishi wa habari za mpira wa miguu, amesema matokeo yanayopatikana sasa hivi ni kwa ajili ya nidhamu iliyowekwa na TFF kuhakikisha wanafanya kazi katika utaratibu.
Karia ameeleza kuwa ni vizuri kila mtu kuheshimu nafasi ya kila mmoja pale anapokuwa kwenye nafasi yake ili kusikilizana na kuepusha mvutano.
“Yeyote ambaye anakupa utaratibu, anashauriana na wewe, anakupa maoni kwa njia ambayo haina masuala ya mvutano, ni rahisi kutekelezwa, sisi ni binadamu,” amesema.
Simba, Yanga kumiliki viwanja vyao ndani ya miezi sita
Aidha, amemtaka kila mmoja kuheshimu mamlaka na utaratibu uliowekwa kwa sababu TFF haitomfumbia macho yeyote atakayeshindwa kufuata taratibu hizo.
“Ukishindana siku zote na mamlaka utakuja utaumia kwa hiyo unatakiwa ufuate mamlaka kama inavyotakiwa au kama unataka ubwabwaje basi ukae pembeni uzungumze ukiwa pembeni lakini ukiwa familia mkono wetu utakushughulikia,” ameongeza.