Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania

0
40

Tanzania ikitarajia kufanya uchaguzi mkuu kesho Oktoba 28, 2020, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres amewasihi wadau wote kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa shirikishi na unafanyika kwa amani.

Amesisitiza kuwa mchakato wote wa uchaguzi unapaswa kuwa jumuishi na kutoa mwanya wa ushiriki kwa vyama vyote na wagombea wao, hasa wanawake katika kuendelea kuimarisha hatua iliyopigwa na Tanzania kuhakikisha utulivu, demokrasia na maendeleo endelevu.

Aidha, amevisihi vya vya siasa na wadau wengine kujiepusha na vitendo vya vurugu, lakini pia mamlaka zihakikishe uwepo wa mazingira rafiki yatakayowaruhusu Watanzania kutimiza haki yao ya kiraia na kisiasa.

Amesema kuwa UN itaendelea kuchochea maendeleo endelevu ya Tanzania na kuhakikisha kizazi kijacho cha Tanzania kinanufaika.

Send this to a friend