Ukaguzi wa magari kufanyika Japan kabla ya kuingia nchini

0
44

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuanzia Julai 20, 2022 utaratibu wa kukagua magari kutoka nchini Japan utafanyika kwenye nchi hiyo kwa kutumia utaratibu wa Pre-shipment Verification of Conformity to standards (PvoC) tofauti na utaratibu wa sasa ambapo magari hukaguliwa baada ya kuwasili nchini kwa utaratibu wa Destination Inspection (DI).

TBS imeeleza kuwa magari yote yatakayosafirishwa kutoka nchini Japan kuanzia Julai 20, yatakaguliwa na wakala EAA Company Limited kwa utaratibu wa PvoC, na magari yote ambayo yalishasafirishwa kabla ya Julai 20, 2022 yatapimwa kwenye bandari ya Tanzania kwa utaratibu wa sasa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa magari mengine yanayotoka nchi tofauti na Japan yataendelea kukaguliwa nchini hadi hapo utaratibu mpya utakapotolewa.

Aidha, shirika hilo limesema litahakikisha magari yote yaliyotumika na kuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha Tanzania cha magari yaliyotumika.

Send this to a friend