Ukomo wa umri wa Urais Uganda, mahakama yatoa uamuzi

0
38

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) imetupilia mbali pingamizi lililokuwa limefunguliwa dhidi ya muswada wa mabadiliko ya Katiba ya Uganda unaolenga kuondoka ukomo wa umri kwa wagombea Urais.

Mwanasheria kutoka nchini humo, Male Mabirizi alifungua kesi hiyo kupinga uamuzi wa mahakama ya juu ya Uganda ambayo iliidhinisha mabadiliko hayo.

Mabadiliko hayo yameondoa kipengele cha sifa za mgombea Urais ambacho kilikuwa kinaeleza kuwa yeyote anayetaka kugombea ni lazima awe na umri kati ya miaka 35 na 75.

Kufuatia mabadiliko hayo na uamuzi huo wa mahakama ni wazi kuwa Rais Yoweri Museveni (76) ataweza kugombea kwa muhula wa sita katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka 2021.

Send this to a friend